SABABU ZA KIZUNGUZUNGU NA TIBA ZAKE

1594203910483.png


BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Wakuu naomba nifikishe kilio cha rafiki yangu mmoja mwenye tatizo la kupata kizunguzungu kila alalapo, hasa anapolala chali kitandani. Huyu jamaa ana umri kati ya miaka 30 - 35, hana historia ya kuvuta sigara, hatumii pombe wala hatumii madawa makali ya aina yoyote .
Watu wanaopata kizunguzungu wana namna mbalimbali za kuelezea dalili zake, mfano:
  • Kuhisi kama kichwa au mwili mzima unazunguuka
  • Hali ya kujisikia kama unataka kupoteza fahamu au kichwa kuwa chepesi
  • Kukosa balance
  • Kuhisi kama unaelea angani au kwenye maji
Dalili                                            
Dalili hizi zinaweza kuanza mara baada ya mtu aliyekuwa amekaa
akaamka kiasi cha kumfanya atulie kwanza kabla ya kuanza kutembea, au
aliyesimama anapotembea, au kugeuza kichwa. Hali ya kizungunguzu mara
nyingi huambatana  na kichefuchefu. Kizunguzungu kinaweza kudumu kwa
sekunde au hata wiki kadhaa na kinaweza kujirudia rudia baadae baada ya
kutulia kwa muda fulani
Sababu za kwenda hospitali
Inashauriwa kumuona daktari utakapoona dalili zinajirudia rudia, au
unapopata kizunguzungu ambacho ni cha ghafla na kikadumu kwa muda mrefu.
Pia kikiambatana na dalili zifuatazo:
  • Maumivu makali ya kichwa
  • Maumivu ya kifua
  • Kupumua kwa shida
  • Ganzi ya ghafla au kupooza kwa miguu, mikono au usoni
  • Kupoteza fahamu
  • Kuona maruweruwe (double double)
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio na au kupiga ovyo ovyo bila mpangilio
  • Kuchanganyikiwa au kuongea kwa shida
  • Kutapika kusikokoma
  • Kujikwaa kwaa bila sababu au kutembea kwa shida
  • Degedege
  • Kutosikia vyema kwa ghafla
Chanzo
Ziko sababu kadha wa kadha zinazoleta kizunguzungu kama matatizo ya
masikio, athari za kusafiri, dawa, magonjwa kama Malaria, magonjwa ya
moyo, shinikizo la damu, Kisukari, na ajali. Jinsi kizunguzungu
kinavyokufanya ujisikie au mambo yanayofanya kianze au muda kinaokuwepo
na dalili zingine zinazoambatana nazo, vyote hivyo hutoa mwanga kwa
daktari kujua chanzo.
Matatizo ya viuongo vya ndani vya sikio.
Uwiano (balance) anaokuwa nao mtu aliye mzima na kumwezesha kutembea
bila kupepesuka unatoka na kazi ya viungo mbalimbali vya hisia vya mwili
wa binadamu. Viungo hivi ni:
  • Macho, kazi yake ni kukuwezesha kujua uko wapi na unatembeaje au kosogea.
  • Mishipa ya fahamu, kazi yake ni kupeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu mwendo na mwili ulipo
  • Sehemu ya ndani ya sikio, Sikio lina sehemu kuu
    tatu, sehemu ya nje ambayo tunaiona kwa urahisi, sehemu ya kati ilipo
    ngoma ya sikio, na sehemu ya ndani kabisa ya sikio ambayo ni baada ya
    ngoma, hii huwa hatuioni kwa macho. Sehemu ya ndani kabisa ya sikio ina
    viuongo ambavyo vinatusaidia kupata uwiano (balance) wa mwili kwa
    kusaidiana na viungo vingine nilivyovitaja hapo juu. Husaidia kujua
    nguvu za uvutano (gravity) na kukufanya ujue kama unaenda mbele au
    unarudi nyuma.
Kizunguzungu cha kuhisi vitu vilivyoko karibu nawe vinazunguuka
kitaalam Vertigo (inatamkwa Vetaigo). Hii husababishwa mara nyingi na
matatizo ya masikio ambapo viungo vilivyo kwenye sehemu ya ndani ya
sikio (Inner Ear) kupeleka taarifa zisizo sahihi kwenye ubongo na hizo
taarifa zinakuwa haziwiani na zile ambazo macho na mishipa imepokea.
Unapata aina hiyo ya kizunguzungu kwakuwa ubongo unakuwa busy kujaribu
kupata ukweli halisi wa hizi taarifa. Aina hii ya kizunguzungu huletwa
na magonjwa yafuatayo:
  • Kizunguzungu kisichofahamika chanzo (Benign Paroxysmal Positional Vertigo)
    – Kizunguzungu hiki hakina athari kubwa kwa maisha ya muhusika. Aina
    hii ya kizunguzungu hakifahamiki chanzo chake (idiopathic), kwa lugha
    nyepesi tungesema cha kuzaliwa nacho. Hutokea pale mtu anapobadili mkao
    ghafla; kuamka na kukaa kitandani ghafla au kusimama ghafla kwa mtu
    aliyekuwa ameketi. Pia kugeuza au kuinamisha au kuangalia juu haraka.
  • Uambukizo; Mishipa ya fahamu ya sehemu ya ndani ya
    sikio inapopata uambukizo wa aina fulani ya virusi na kusababisha
    kizunguzungu na wakati mwingine hata kutosikia sawa sawa.
  • Kujaa kwa majimaji sehemu ya ndani ya sikio (Meniere’s disease); hapa
    tunamaanisha maji yanayotengenezwa ndani ya sikio kwasababu fulani
    fulani huzidi kiwango kinachokubalika na kusababisha kizunguzungu
    ambacho hudumu kwa masaa kadhaa. Pia huleta kuziba na kuzibuka kwa
    masikio, sauti za kengele na kuhisi kama vile sikio limezibwa kwa pamba.
  • Kipanda uso (Migraine). Watu wanaopata matatizo ya
    kipanda uso hupata pia kizunguzungu hata kama kwa wakati huo kichwa
    hakiumi. Kizunguzungu wanachopata hawa huwa kina dumu kwa dakika hadi
    saa kadhaa na kupotea. Pia wanakuwa na hali ya kutotaka makelele, sauti
    ndogo wao huhisi ni kelele kubwa sana.
Matatizo ya mzunguuko wa damu unavyoweza kuleta Kizunguzungu
  • Kushuka kwa shinikizo la damu (Low Pressure). Kushuka
    kwa ghafla kwa shinikizo la damu kunaleta kizunguzungu cha muda mfupi.
    Hali hii inaweza kutokea iwapo utasimama ghafla kama ulikuwa umeketi au
    kuamka na kuketi kitandani ghafla. Kubadilika kwa mkao wa mwili huku
    kunasababisha shinikizo la damu lishuke ghafla kwani mwili unakuwa
    haujapata muda wa kujiweka sawa.
  • Matatizo ya kutozunguuka vyema kwa damu; huku
    kunatokea kwa watu wenye magonjwa ya moyo kuwa mkubwa (Cardiomyopathy),
    shambulio la moyo (Heart attack), na mapigo ya moyo yaliyoparaganyika
    (Arrhythmia). Matatizo haya yote yanababisha moyo ambao ndiyo pump,
    kupungua uwezo wa kusukuma damu ya kutosha kwa ajili ya mahitaji ya
    mwili, ikiwemo ubongo na sehemu ya ndani ya sikio.
Sababu zingine zinazoleta kizunguzungu
  • Magonjwa ya mishipa ya fahamu
  • Dawa zinazotumika kutibia matatizo mbalimbali
    yanaweza kuwa chanzo cha kizunguzungu. Mfano dawa za kuzuia degedege,
    dawa za sonona, na dawa za kutibu shinikizo la damu pia huwa ni sababu
    kwani kuna wakati hushusha shinikizo la damu kufikia chini ya kiwango.
  • Aina fulani ya magonjwa yanayomfanya mtu kuwa na wasiwasi kuliko kawaida huleta kizungunguzu.
  • Upungufu wa damu. Kupungua kwa wekundu wa
    chembechembe nyekundu za damu huleta kizungunguzu kwani kiwango cha hewa
    ya oxygen kinachozunguuka kinakuwa kidogo.
  • Kushuka kwa sukari. Hali hii huwapata watu wenye
    kisukari wanaotumia insulin ambayo inaweza kusababisha sukari kushuka
    sana. Pia hata wenye njaa kupita kiasi.
  • Joto kali na kupungukiwa maji. Joto kali husababisha kutokwa na jasho jingi hivyo maji mwilini kupungua na kuleta kizunguzungu.
Athari
Athari kubwa za kizunguzungu zinakuja pale ambapo kizunguzungu
kinapoweza kusababisha muhusika kuanguka chini. Kitendo cha kuanguka
kinaweza kuleta majeraha mbalimbali mwili kulingana na namna na mahala
alipoangukia muhusika. Athari nyingine ni za kiuchumi na kijamii pale
ambapo kizunguzungu kikiwa cha muda mrefu na kusababisha muhusika
ashindwe kushiriki shughuli za kumuingizia kipato na za kijamii.

DAWA ZINAZOSABABISHA KIZUNGUZUNGU

Orodha ya dawa ambazo athari ni kizunguzungu, inexhaustible. Hizi ni pamoja na:
  • analgesics (maumivu relievers);
  • dawa antianginal;
  • vipunguza;
  • beta blockers,
  • diuretics;
  • moyo glycosides,
  • antibiotics,
  • nonsteroidal kuzuia uvimbe madawa,
  • antidepressants,
  • tranquilizers,
  • hiponoti,
  • kinza msukosuko;
  • ototokchisnostyu hasa ina idadi ya antibiotics, aminoglycosides - "streptomisini", "kanamycin", "neomycin".

Utambuzi
Utambuzi wa matatizo yanayoleta kizunguzungu yatahusisha uchukuaji wa maelezo na kufanya vipimo ambavyo daktari ataona vinafaa.

Matibabu
Yatategemeana na chanzo kilichogundulika. Matibabu yanaweza kuhusisha dawa, upasuaji na mazoezi

MBINU WATU TIBA

Kwa pamoja na madawa ya kulevya eda na daktari kuhudhuria, unaweza kutumia njia za dawa za asili. Wakati anapata giza katika macho na kizunguzungu, Wao kusaidia zawadi ya asili.

MCHANGANYIKO WA MIMEA

Kwa ajili ya matibabu ya kisulisuli Unaweza pia kutumia chamomile maua, maua, lemon zeri na Valerian mizizi kwa idadi sawa. kijiko ya muundo huu pombe maji ya moto katika beakers mbili. Kusisitiza maana usiku mmoja na asubuhi ya kuongeza vijiko viwili vya asali na kiasi hicho cha siki apple cider. Kuchukua dawa kusababisha juu ya tumbo tupu nusu saa kabla ya milo mara mbili kwa siku. muda wa matibabu hii ni wiki mbili.
madawa kutoka kizunguzungu kwa wazee

TANGAWIZI

Ginger mizizi hupondwa na unga mzuri na katika hili matumizi ya serikali ndani ya robo kijiko mara tatu kila siku na maji moto. Kama unajisikia kizunguzungu na huzuia dhaifu kazi, basi hii ni chaguo bora, kwa sababu tangawizi tani na kuboresha utendaji.

HAWTHORN

hawthorn Grass sana kutumika kutibu matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa mishipa, spasm maana kabisa kuondosha mishipa misuli na tani. Kutengeneza dawa za lazima zilizokusanywa katika inflorescence ukubwa tablespoons nne, saga yao ndani ya unga na kumwaga lita moja ya maji ya moto. Kupenyeza kwa dakika kumi na tano ya kula mara tatu kwa siku kabla ya milo.

VITUNGUU

Kila mtu anajua athari ya uponyaji wa vitunguu. vitu ni pamoja na ndani yake, na antimicrobial, antiviral na tonic mali. Bora ya kula vitunguu pamoja na tangawizi. Ili kufanya hivyo, saga vitunguu katika chesnokodavke, tangawizi, wavu, kuchanganya viungo hizi mbili na changanya vizuri. Kula ndani ya kijiko, unaweza kuongezwa kwa chakula kama kitoweo.
ghafla kizunguzungu

HITIMISHO

Kama uzoefu dalili kizunguzungu lazima mara moja kushauriana daktari kwa utawala wa nje ugonjwa mbaya. Kufanya madawa wao wenyewe kutoka kizunguzungu kwa wazee haipendekezwi kuzuia maendeleo ya ugonjwa huo. Inahitajika mashauriano ya neurologist, otolaryngologist, mtaalamu. Kuwa na afya!
SABABU ZA KIZUNGUZUNGU NA TIBA ZAKE SABABU ZA KIZUNGUZUNGU NA TIBA ZAKE Reviewed by Cadotz media on August 24, 2020 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA