Miujiza ya papai kiafya na mbegu zake
Masele afichua utetezi dhidi ya wanyonge umempatia umaarufu
Naibu Spika amtetea mbunge aliyechana hotuba ya upinzani
Rugemalira aomba uamuzi Mahakama Kuu utenguliwe
Adaiwa kumuunguza mjukuu wake kisa kukojoa kitandani
HABARI KUBWA
Pamoja na matumizi hayo, wengi hula wakijua ni kama yalivyo matunda mengine bila kujua kama yana manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.
Aidha, wengine hutumia kama kinywaji kwa maana ya juisi ikiwa peke yake au kwa kuchanganywa na matunda mengine kama vile embe na kufanya juisi mseto. Wengine pia huchanganya papai na matunda mengine kwa kufanya mseto huo pamoja na karanga na tende. Yote hiyo ni kuleta vionjo tofauti katika kinywaji hicho laini.
Inawezekana watu wanatumia tunda hilo kwa namna tofauti bila kuelewa yaliyomo ndani yake kwa habari ya afya.
Wataalamu wa masuala ya afya na lishe wanabainisha kuwa tunda hilo ni mujarabu kwa afya ya mwandamu.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘organicfact.net’ ambao hutoa elimu juu ya nafasi ya vyakula mbalimbali ikiwamo mboga na matunda kwa afya ya binadamu, wamebainisha kuwa papai lina manufaa makubwa katika mwili wa binadamu kutokana na kusaidia kumeng’enywa kwa chakula.
“Uwapo wa mmeng’enyo maarufu kama ‘papain’, husaidia kurahisishwa kwa mmeng’enyo wa chakula kwa kuvunjavunja vyakula vya aina ya protini pamoja na kusafisha mfumo mzima wa chakula,” unaeleza mtandao huo.
Inabainishwa kuwa hatua hiyo hupunguza wingi wa protini mwilini ambayo huchangia mafuta katika mwili kuongezeka na hivyo kuwezesha hata mafuta kupungua.
“Kama protini kwenye vyakula vinavyotumiwa na mwanadamu itakuwa nyingi, mlaji anaweza kukumbwa na matatizo katika mfumo wa chakula, kisukari, shinikizo la damu la juu na matatizo mengine kiafya.”
KUPUNGUZA UZITO
Habari njema kwa afya kutokana na matumizi ya papai ni pamoja na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza uzito.
“Mapapai pia ni mazuri kwa afya hasa kwa wale wenye uzito uliozidi kwani kwa kula matunda hayo hupunguza uzito haraka. Kula bakuli la mapapai asubuhi au jioni ni muhimu kwa afya yako.”
Faida nyingine za mapapai ni pamoja na uwezo mkubwa katika kupambana na minyoo tumboni, hivyo kupunguza uwezekano wa mtu kukumbwa na maambukizi na maradhi mengine yatokanayo na mfumo wa tumbo.
TIBA YA MENO
Wataalamu wanabainisha pia kuwa papai ni tiba kwa meno ya mwanadamu. Inaelezwa kuwa mtu mwenye tatizo la meno, anaweza kuchukua kipande cha papai na kusugua katika sehemu ya jino au fizi inayouma na hatimaye kupata nafuu.
Pia inaelezwa kuwa papai ina fasida kubwa katika kuimarisha ngozi ya binadamu ndiyo maana imekuwa ikitumika katika kutengeneza vipodozi mbalimbali.
Mbali na kutumika kwenye vipodozi, papai pia hutumiwa na wanawake wengi kwa kujipaka ikiwa ni sehemu ya kuimarisha afya ya ngozi. Kwa matumizi hayo, inaelezwa kuwa hutibu baadhi ya maradhi ya ngozi pamoja na kuondoa vipele na chunusi na kuufanya mwonekano wa sura na ngozi kuwa freshi.
Wataaamu wa afya ya ngozi pia wanabainisha kuwa kwa kutumia papai huufanya mwili hususan ngozi kuwa imara dhidi ya madhara yatokanayo na mtu kuungua jua.
Aidha, kwa watu wanaotumia kufanya ‘massage’ kwa kutumia papai wanafaidika kiafya kutokana na tunda hilo kuua seli zilizokufa. Inaelezwa kuwa papai huifanya ngozi kuwa nyororo na hutibu magonjwa kadhaa ya ngozi.
KUDHIBITI SARATANI
Kwa wale wanaosubuliwa na maradhi ya saratani au hawajakumbwa nayo, watafiti wanaeleza kuwa tunda hilo ni kinga kwa tatizo hilo ambalo limekuwa sugu na chanzo cha mauaji ya mamilioni ya watu duniani.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, utafiti uliofanywa na wanasayansi mbalimbali umeonyesha kuwa papai lina uwezo mkubwa katika kudhibiti maradhi ya saratani za aina mbalimbali ikiwamo ile ya titi.
Wataalamu hao wanabainisha kupitia utafiti huo kuwa jani la papai hasa kavu hutengeneza kinga maarufu kama ‘anti-carcinogenic’ ambazo hupambana
TIBA YA MACHO
Wataalamu wa tiba lishe pia wanaelezea kuwa mapapai ni kinga murua kwa macho hasa maradhi maarufu kama ‘m acular degeneration’ ambayo husababisha baadhi ya seli katika macho na kusababisha uoni hafifu na hata upofu kabisa.
Aina ya ugonjwa huo, kwa mujibu wa wataalamu, huwakumba watu wenye umri mkubwa hivyo kwa kutumia papai husaidia kupunguza uwezekano wa kukumbwa na maradhi hayo.
Sambamba na hiyo, papai kama ilivyo karoti, lina ‘beta-carotene’ ndiyo maana lina rangi ya njano
hivyo huimarisha uoni wa macho na hata upofu.
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na jarida la ‘Archives of Ophthalmology’, kula papai mara mbili au tatu kwa siku kuna uwezekano wa kupunguza au kuepusha mtu kukumbwa na tatizo la macho.
Vile vile watu wenye tatizo la kukosa choo wanaelezwa kuwa utumiaji wa papai mara kwa mara huwaepusha na janga hilo la kiafya.
Hiyo ni kutokana na papai kuwa na ‘folate’, vitamini C na E ambayo husaidia kuufanya utumbo kuwa katika hali bora.
KWA KINAMAMA
Baadhi ya kinamama wamekuwa wakikumbana na matatizo ya tumbo wakati wa hedhi. Habari njema kwao ni kwamba matumizi ya juisi ya papai yanaweza kuwaweka huru dhidi ya tatizo hilo.
“Pia utumiaji wa papai kijani au ambalo halijaiva sawasawa unaweza kumfanya mwanamke kutokuwa na matatizo katika mzunguko wake wa hedhi,” utafiti wa wanasayansi unabainisha.
Papai pia huuelezwa na wataalamu kuwa ni ‘chakula moto’ kwa maana kuwa huzalisha joto mwilini na uzalishaji huo wa joto husaidia kuzifanya homoni kuwa changamfu.
Hii inahusisha pia vipindi vya kinamama kuwa katika hedhi, hivyo husaidia kumfanya kuwa katika hali nzuri kiafya wakati huo.
FAIDA ZA KIAFYA ZA TUNDA LA
PAPAI
Tunda la papai lina faida nyingi
sana kwa afya ya mwanadamu.
Miongoni mwa faida hizo ni
pamoja na kuwa na uwezo wa :
Mbegu za Papai
1. Kutibu tatizo la kusaga
chakula tumboni
2. Kutibu Udhaifu wa tumbo
3. Kutibu Kisukari na asthma au
pumu.
4. Kutibu Kikohozi kitokacho
mapafuni
MIZIZI YA PAPAI
5. Kutibu Kifua kikuu
6. Tunda hili huleta afya nzuri
ukitumia kila siku
7. Maziwa yanayotoka katika
jani lake huponya vidonda
8. Vilevile yanasaidia kutibu
sehemu iliyoungua moto
9. Kama hiyo haitoshi, maziwa
yanayotoka katika jani la mpapai
yanatibu kiungulia na Ugonjwa
wa colon (njia ya haja kubwa
kwa ndani)
MAJANI YA MPAPAI
10. Pia yanasaidia kutofunga
choo
11. Maganda ya tunda la papai
yanasaidia kutibu tatizo la
kuungua, vipele na saratani ya
ngozi.
12. Mbegu zake zinatibu ini
zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.
13. Majani yake yakaushie ndani,
yanatibu pumu.
Inapoanza kubana yachome
majani yaliyokaushwa kisha
jifukize, kule kubanwa
kutakisha.
14. Majani yake yanasaidia
katika kutibu shinikizo la damu.
15. Papai likimenywa na
kupondwa linafaa Sana katika
masuala ya urembo, kwani
linaweza kutumika Kama vile
unavyotumia lotion kulainisha
uso.
16. Mbegu za papai zina uwezo
wa kutibu homa.
Meza mbegu za papai kiasi cha
kijiko cha chakula mara 3 kwa
ajili ya kutibu homa.
17. Mbegu za papai
zilizokaushwa ndani kisha
zikasagwa na kua unga zinatibu
malaria,
Tumia kijiko 1 cha chai
changanya na uji, kunywa mara
3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua
kikuu akila matunda haya kwa
muda mrefu atapona bila dawa
nyingine.
18. Mizizi yake ikipondwa na
kulowekwa katika maji
yaliyochemshwa, lita 2 na nusu
kwa dakika 15, inatibu figo,
bladder, inazuia kutapika. Nusu
kikombe cha chai kutwa mara 3
kwa siku 5.
Miujiza ya papai kiafya na mbegu zake
Reviewed by Cadotz media
on
June 25, 2019
Rating:
Post a Comment