Rangi Ya Mkojo Wako Inasema Kitu Gani Kuhusu Afya Yako?

Mwili una mifumo mbalimbali ambayo hushirikiana kwa karibu katika ufanyaji kazi. Mara nyingi matatizo katika mfumo fulani huweza kuonekana katika mabadiliko kadhaa ya kimwili ambayo huweza kuonekana nje ya mwili.

Mkojo ni moja ya viashiria vya matatizo mbalimbali mwilini hasa matatizo katika mfumo wa mkojo.

Zifuatazo ni rangi za mkojo na maana zake katika Afya ya mhusika.
1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi)
Unakunywa maji mengi kupita kiasi. Ikiwezekana unashauriwa upunguze kidogo

2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo
Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.

3. Manjano iliyopauka
Upo kawaida tu

4. Njano iliyokolea
Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji baada ya muda mfupi

5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali
Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa.

6. Rangi ya Kahawia
Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kama hali hii ikiendelea.

7. Rangi ya Machungwa yaliyoiva
Una upungufu wa maji mwilini au uwezekano wa matatizo katika ini au mfuko wa nyongo hivyo umuone daktari. Inaweza kutokana na rangi ya chakula pia(food dye).

8. Rangi ya bluu au kijani
Inaweza kusababishwa na rangi za chakula, athari za dawa au ishara ya maambukizi ya bakteria. Muone daktari endapo itaendelea kwa muda mrefu.

9. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu
Kama hujala matunda yoyote nyenye asili ya uwekundu, basi huwenda una Damu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugonjwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.

10. Mkojo wenye mapovu
Inaweza kuwa ishara ya matatizo ya figo au protini zilizozidi mwilini. Muone daktari endapo inakutokea mara kwa mara.

11. Rangi nyingine(ukiondoa zilizotajwa juu)
Inaweza kusababishwa na rangi za chakula, dawa au kemikali nyingine. Kama huna uhakika ni vyema kumuona daktari.
Rangi Ya Mkojo Wako Inasema Kitu Gani Kuhusu Afya Yako? Rangi Ya Mkojo Wako Inasema Kitu Gani Kuhusu Afya Yako? Reviewed by Cadotz media on August 25, 2020 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA