Magonjwa ya Zinaa -No-4


Ugonjwa wa Kaswende

Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Ugonjwa wa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi.

Dalili na Viashiria vya ugonjwa wa kaswende
Dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende hutegemea na aina ya ugonjwa wa kaswende wenyewe. Kuna aina tano za ugonjwa wa kaswende ambazo ni;
Ugonjwa wa kaswende wa awali (Primary syphilis)
Ugonjwa wa kaswende wa pili (Secondary syphillis)
Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)
Kaswende ya kurithi (Congenital syphilis)
Kaswende ya awali (primary syphilis)
Dalili ya kwanza ya aina hii ya kaswende ni kutokea kwa kidonda kidogo cha mviringo (chancre kama kinavyojulikana kitaalamu) katika sehemu ambayo bakteria wameingilia na hutokea kati ya siku 10 hadi miezi mitatu (kwa kawaida kuanzia wiki 2 hadi 6) baada ya mtu kupata maambukizi ya kaswende. Kidonda hiki kinaweza kutokea kwenye sehemu ya haja kubwa, shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mdomoni (lips), uume (penis), ulimi, vulva, tupu ya mwanamke (vagina) na sehemu nyengine mwilini.
Tezi (lymph nodes) ambazo zipo karibu na sehemu iliyotokea kidonda hiki kawaida huwa zinavimba baada ya siku 7 hadi 10. Kidonda hiki hakiambatani na maumivu na kwa kuwa kinaweza kutokea katika sehemu zilizojificha kama kwenye shingo ya kizazi, sio rahisi mtu kutambua kama na aina hii ya kaswende. Kidonda hiki kinaweza kuwepo kwa muda wa wiki 3 hadi 6 kama mtu hatapata tiba na kinatoweka chenyewe bila tiba au baada ya kupata tiba.
Robo tatu ya wale ambao hawapati tiba huishia kuingia kwenye kundi la kaswende ya aina ya pili (Secondary syphilis).
Kaswende aina ya pili (Secondary syphilis)
Aina hii hutokea wiki 4 hadi 10 baada ya mtu kupata kaswende ya awali. Dalili za aina hii ya kaswende ni;
Vipele ambavyo haviwashi katika viganja vya mikono au nyayo za miguu. Vipele hivi pia vinaweza kutokea mwili mzima au sehemu mbalimbali za mwili.
Uchovu
Kuumwa kichwa
Homa (fever)
Kunyofoka nywele
Vidonda vya koo (sore throat)
Kuvimba kwa matezi mwili mzima
Maumivu ya mifupa (joint pain)
Kupungua uzit




Magonjwa ya Zinaa -No-4 Magonjwa ya Zinaa -No-4 Reviewed by Cadotz media on June 14, 2019 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA