Magonjwa ya Zinaa -No-3


Madhara ya ugonjwa wa kaswende katika mfumo wa mishipa ya fahamu hutokea miaka 10-20 baada ya mtu kuugua ugonjwa wa kaswende na ambaye hakupata tiba yoyote hapo awali. Madhara haya huonekana kwenye uti wa mgongo na kwenye ubongo.
Kuna aina nne ya neurosyphilis kama ifuatavyo
Isiyo na dalili (Asymptomatic) – Katika aina hii mgonjwa anakuwa hana dalili zozote. Aina hii ndio huonekana sana kwa wagonjwa ambao hawakupata tiba hapo awali.
Ulemavu wa jumla (General paresis)
Inayoshambulia tando za ubongo na mishipa ya damu (Meningovascular)
Inayoshambulia sehemu za chini za uti wa mgongo (Tabes dorsalis)
General paresis hutokana na kuathirika kwa ubongo na hivyo kuleta upungufu katika ufanyaji kazi wa ubongo (impairement of mental function). Aina hii pia huweza kutokea kwa wagonjwa wa kisonono (gonorrhoea).
Dalili za general paresis
Kupungua uwezo wa kuzungumza (aphasia)
Kupungua uwezo wa kufanya maamuzi (impaired judgement)
Kutokuwa na uwezo wa kuhesabu kitu chochote
Kupungua kuhamasishika (impaired motivation)
Kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vilivyopita muda mrefu (loss of long term memory)
Kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vilivyopita karibuni/muda mfupi (loss of short term memory or recent events)
Degedege
Kushindwa kutembea au kutumia miguu, mikono na viungo vyengine vya mwili
Mabadiliko ya kitabia na kihisia (personality changes) kama
Delusions, kuona au kusikia vitu ambavyo visivyokuwepo (hallucinations)
Kukasirika kwa haraka (irritability)
Inappropiate moods
Low mood
Viashiria vya general paresis
Mboni za jicho kuwa katika umbile ambalo si la kawaida
Mboni kushindwa kupepesuka (changes in pupil response)
Kupoteza uwezo wa kuhisi mgandamizo au mtikisiko katika ngozi (Loss of sense of vibration or position)
Kushindwa kusimama wakati mtu amefunga macho (romberg test)
Kushindwa kutembea vizuri
Viungo vya mwili kuwa dhoofu
Matatizo ya kusahau
Vipimo vya uchunguzi
FTA- ABS – Kipimo cha damu kinachofanya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum wanaosababisha kaswende
RPR (Rapid Plasma Reagin) – Kipimo hiki pia huangalia antibodies za Treponema Pallidum katika damu ya wagonjwa wa kaswende
VDRL (Veneral Disease Research Laboratory)- Kipimo cha kuangalia antibodies za Treponema Pallidum, kipimo hiki kimeshahabiana sana na kipimo cha RPR.
Lumbar Puncture – Kipimo cha kuchukua maji ya uti wa mgongo ili kuangalia kiwango cha sukari katika maji hayo, presha yake, protini, chembechembe nyekundu na nyeupe za damu, rangi yake, madini ya chloride. Kipimo hiki ni muhimu sana kwani husaidia kutambua kama kuna magonjwa mengine kama ugonjwa wa uti wa mgongo, multiple sclerosis, hypoglycemia, kiharusi, saratani, jipu nk.
Cranial CT na MRI – CT Scan ya kichwa pamoja na kipimo cha MRI ili kuangalia kama kuna magonjwa mengine mbali na kaswende na kuangalia sehemu ipi ya ubongo iliyoathirika.
Nerve conduction test – Kipimo cha neva za mwilini
Vipimo vya macho
Dalili za meningovascular ni
Mboni kuwa ndogo
Kupooza kutokana na kuathirika kwa neva mbalimbali
Kuharibika mishipa ya damu mwilini
Kupooza upande mmoja wa mwili
Matatizo ya kumeza chakula – Kumeza chakula kwa shida
Degedege
Kupooza neva ya jicho (optic neuropathy)
Matatizo ya macho (chorioretinitis)
Ukiziwi
Vertigo nk.

Vipimo vya uchunguzi vya meningovascular
1. Vipimo vya hepatitis
2. ELISA for HIV – Kipimo cha ugonjwa wa ukimwi
3. PCR (Polymerase Chain Reaction) – Kipimo cha kuangalia vina saba vya bakteria mbalimbali kama Chlamydia trachomatis, Trichomonas vaginalis nk.
4. Urinalysis (urine test) – Vipimo vya mkojo
5. Tabes Dorsalis husababisha kudhoofika kwa viungo vya mwili kutokana na kuathirika kwa uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu. Hali hii ni hatari sana kwani ina kawaida ya kuwa endelevu na huweza kusababisha kifo kwa mgonjwa.
Dalili za Tabes Dorsalis
Kutembea kwa shida
Mgonjwa kutembea huku ametanua miguu sana (wide based gait)
Kudhoofika viungo vya mwili
Kupoteza uwezo wa kuunganisha hisia na matendo fulani fulani katika mwili (Loss of coordination)
Kuwa na hisia zisizo za kawaida mwilini kama vile kujihisi vitu vinachoma choma (lightening pains)
Loss of reflexes
Vipimo vya uchunguzi vya Tabes Dorsalis
CBC (Complete Blood Count) – Kipimo cha wingi wa damu, kuangalia aina za chembechembe za damu nk.
Urinalysis – Kipimo cha mkojo
Lumbar Puncture for CSF – Kipimo cha kuangalia maji ya uti wa mgongo kama nilivyoeleza hapo juu.
CT Scan – Kipimo cha CT Scan ya kichwa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu.
MRI ya kichwa
VDRL, RPR, FTS-ABS, MHA-TP – Vipimo vya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum kama nilivyowahi kueleza.
Tiba ya Neurosyphilis
Tiba ya aina zote za neurosyphilis huusisha kwanza kutibu ugonjwa wa kaswende kwa kutumia dawa za antibiotics aina ya penicillin G au doxycyline kwa wale wanaopata madhara ya penicillin. Hata hivyo kwa wale wenye matatizo na penicillin ni bora kumueleza Daktari mapema ili achukue hatua zinazostahili.
Kwa wale wagonjwa wasioweza kula, kuvaa nguo, wale waliopooza viungo, wasioweza kuzungumza, watahitaji tiba mbalimbali kama rehabilitation therapy, physical therapy, occupation therapy, speech therapy nk.

Magonjwa ya Zinaa -No-3 Magonjwa ya Zinaa -No-3 Reviewed by Cadotz media on June 14, 2019 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA