TIBA ZA ASILI ZA KUONDOA M’BA

Hakuna kitu kina tia aibu na kuweza kukudhalilisha kama m’ba kwa maana kuzuia kujikuna ni mara chache sana kwa jinsi unavyo washa, sasa imagine upo sehemu za watu halafu unaanza kukuwasha. Na kwa fikra zetu waafrika huwa tuna dhani m’ba una sababishwa na uchafu basi ni madharirisho mara mbili kwamba wewe ni mchafu, lakini mba hasa husababishwa na ukavu wa ngozi au fungal infection. Una weza kutumia shampoo za kuondoa mba lakini zina ma kemikali ambayo yanaweza kukuletea matatizo ya ngozi ni afadhali ukatumia njia za asili kuwa na sisi kujua ni njia gani


Maji ya limao (juice ya limao)

Limao ni njia moja wapo rahisi ya kuondoa mba bila kupatwa na madhara, citric acid iliyopo katika limao ina saidia kushambulia flake zinazo sababisha fangasi na ina saidia kupandisha ngozi zilizo kufa juu na kukuwezesha kuzisafisha (kuziosha) kwa urahisi.

Njia nzuri ya kutumia Limao kuondoa mba ni kwa kufuata process hizi mbili kwanza kamua kijiko kimoja cha limao bila kutia chochote (undiluted) halafu massage ngozi yako ya kichwa kwa kutumia maji hayo na uache kwa dakika tano. Halafu, step ya pili osha nywele zako kwa kutumia maji ambayo ume changanya na kijiko kimoja cha limao.
Fanya hivi kila unapo taka kuosha nywele.


CHUMVI

Hakuna asiyr nayo kwake basi hii pia ni njia nyingine ya kuondoa mba kichwani mwako, chukua chumvi kisha massage katika kichwa jaribu kufanya hivi kabla huja tumia njia nyingine ya kuondoa mba kisha tumia njia nyingine hii itasaidia kuipa njia yako ya pili kuwa effective mara mbili (Salt)


KITUNGUU SWAUMU

Namna nyingine ya kuondoa mba ni kwa kutumia kitunguu swaumu, una weza kuwaza kuhusu harufu lakini hii nni njia nzuri mno ya kuondoa mba kwa maana ina antifungal properties ambazo zina nguvu kubwa za kuondoa/kusafisha mba kwa haraka., twanga kitunguu swaumu chako na changanya na kikombe kimoja cha maji. Massage katika ngozi ya kichwa iache kwa muda wa dakika kumi kisha osha na shampoo
TIBA ZA ASILI ZA KUONDOA M’BA TIBA ZA ASILI ZA KUONDOA M’BA Reviewed by Cadotz media on June 23, 2019 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA