Je, faida ya tangawiz ni nini?

Tangawizi ina faida nyingi sana kwa mwili wa mwanadamu. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo :
Je, faida ya tangawiz ni nini?


1. Huondoa sumu mwilini haraka sana

2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi

3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi

4. Huondoa uvimbe mwilini
5. Huondoa msongamano mapafuni

6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake

7. Huondoa maumivu ya koo

8. Huua virusi wa homa

9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini

10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)

11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-
LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”


13. Hutibu kansa

zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)

14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)

15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo

17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi

18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi

19. Huongeza msukumo wa damu

20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo

21. Huzuia damu kuganda

22. Hushusha kolesto

23. Husafisha damu

24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa

25. Hutibu shinikizo la juu la damu

26. Husafisha utumbo mpana

27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma

28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI

29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu

31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu

32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa

33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula
34. Husaidia kuzuia kuharisha

35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu

36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto

37. Hutibu homa ya kichwa
38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi

39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito

40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)

41. Huimarisha afya ya figo

42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi

43. Ina madini ya potassium ya kutosha

44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha

46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium

47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene

48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita


JAM YA TANGAWIZI.

Unaweza kutumia Jam ya Tangawizi kujitibu magonjwa mbalimbali kama ilivyo onyeshwa hapo juu.


JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA TANGAWIZI.

Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.


MUONGOZO WA KUJITIBU MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUTUMIA TANGAWIZI.

Unaweza kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao la Tangawizi kwa kufuata maelekezo yafuatayo :


KUJITIBU TATIZO LA KUVIMBIWA NA KUKOSA HAMU YA KULA.

Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.
Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.


KUJITIBU TATIZO LA MAUMIVU YA KUKOO NA KUKAUKA SAUTI

Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.


KUJITIBU TATIZO LA KUHARISHA.

Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.


KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA

Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.


MAUMIVU YA KICHWA CHA WASIWASI

Changanya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.


MAUMIVU MAKALI YA TUMBO

Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.


BARIDI YABISI SUGU

Changanya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.


KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWA

Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu




Je, faida ya tangawiz ni nini? Je, faida ya tangawiz ni nini? Reviewed by Cadotz media on February 05, 2019 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA