Faida za iliki kiafya

Iliki ni kiungo cha tatu kuuzwa kwa gharama duniani.
1. Zaffron
2. Vanilla
3. Cardamom

🏠Iliki ni zao la biashara na kilo moja ya iliki hufukia Tsh 30,000 -35,000
Iliki husaidia sana mzunguko wa damu mwilini, kule inakolimwa kila chakula huwekwa iliki kuanza mihogo ya nazi mpaka wali maharage.

🏠Iliki inadhibiti vidudu vinavyoozesha chakula. Maandazi ya iliki yana maisha marefu zaidi.

🏠Ndiyo maana wanaume wa Pwani hawana hasira. Ilikuwa husaidia ku control moods.

🏠Iliki ni natural antibiotic inayotibu kuanzia UTI mpaka gonorrhoea. Basi kama umeligonga gono usianze kutafuna iliki pata ushauri wa daktari kwanza.


FAIDA ZA HIRIKI KIAFYA:

🏠Hiriki ni kiungo maarufu Sana nchini India, kimekuwa kikitumika kuongeza radha katika vyakula na vinywaji mbali mbali pamoja na dawa za ayuverda.


🏠Kiungo hiki kimetapakaa na kupata kujulikana na kutumika pia sehemu mbalimbali ulimwenguni kutokana na uzuri wa harufu na radha yake

🏠Matumizi katika vyakula ni mengi tukihasabu asilimia 99 ya watu ulimwenguni tunatumia sana kiungo hiki ila wengi wetu hatujui kuwa mbali na hiriki kuwa kiungo katika chakula kuna faida nyingi za kiafya unaweza kupata kwa kutumia kiungo hiki.

🏠Hiriki ni chanzo kizuri cha madini mwilini kama vile madini ya pottassiun, calicium,sulfur, iron pamoja na manganese.

Pia hiriki ina utajiri wa vitamins nyingi sana ambazo ni muhimu sana kata afya yetu ya mwili, vitamini vinavyopatikana katika hiriki ni kama vile vitamin A,B na C,Niacin, na Riboflavin.


ZIFUATAZO NI BAADHI YA FAIDA ZA HIRIKI KIAFYA:-

1. Kuondoa harufu mbaya katika kinywa

🏠Hiriki ina viashiria ambayo vinaweza kuuwa vijidudu vinavyosababisha harufu mbaya katika kinywa.

🏠Tafuna hiriki kila baada ya mlo ili kuacha kinywa chako kikiwa fresh na harufu nzuri.

🏠Sukutua kinywa chako kwa maji ya vuguvugu ya hiriki mara mbili kwa siku,ili kuondoa tatizo la harufu katika kinywa


2. Hiriki Inahimarisha afya ya mfumo wa kusaga na kusharabu chakula na pia inachochea uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kuyeyusha vyakula vyenye mafuta mengi mwilini hii usaidia kupunguza gas tumboni, kuondoa kiungulia na kutibu maumivu ya tumbo

🏠Pendelea kutia hiriki katika vyakula au kunywa sana chai ya hiriki kuhimarisha usagaji wa chakula


3. Hiriki inasaidia kuleta hamu ya kula:-

🏠Kutokana uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kunyeyusha vyakula vya mafuta na virutubisho vingine pamoja na kuondoa gas vitu ambavyo vinachangia kuondoa hamu ya kula

🏠Tia unga wa hiriki katika supu au tafuta mbegu zake ili kurudisha hamu ya kula

4. Hiriki inasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mapafu na kuzibua mirija ya hewa hivyo kuwapa unafuu wenye matatizo ya pumu, na matatizo mengine ya upumuaji

🏠Tumia hiriki kwa kutafuna kwa kiasi au kwa kunywa kusaidia matatizo ya pumu Kama vike kifua kubana na kukohoa.


5. Hiriki inaondoa maumivu ya kichwa yanayotokana na tatizo la usagaji wa chakula.

🏠Kunywa kikombe kimoja cha chai ya hiriki kuondoa maumivu ya kichwa.

🏠Share na marafiki nao wanufaike na elimu hii.
Assalaam Alaykum!

Faida za iliki kiafya Faida za iliki kiafya Reviewed by Cadotz media on February 05, 2019 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA