Muwasho au maumivu kwenye njia ya haja kubwa
Bawasiri ni uvimbe wa mishipa ya damu kwenye njia ya haja kubwa. Huonekana kutuna au kujaa kama jipu karibu na unyeo. Inaweza kutoa muwasho, hisia ya kuungua, au maumivu; hasa wakati wa kujisaidia. Wakati mwingine bawasiri hupasuka na kutoa damu kidogo nyekundu inayong’aa kwenye kinyesi.
Bawasiri ni tatizo la kawaida wakati wa ujauzito na miongoni mwa watu wanaokaa au kubeba mizigo mikubwa kutwa nzima, lakini kila mtu anaweza kuupata. Maumivu kutokana na bawasiri huzidi zaidi mgonjwa anapokuwa na tatizo la choo kigumu, kwa sababu kukitoa choo kigumu hulazimisha mishipa kwenye njia ya haja kubwa kupanuka zaidi.
Matibabu
- Epuka tatizo la ugumu wa choo na bawasiri kwa kujenga tabia ya kunywa maji mengi, kula matunda kwa wingi na nafaka nzimanzima ambazo hazijasindikwa.
- Baadhi ya juisi kutokana na mimea chungu ikipakwa kwenye bawasiri husaidia uvimbe kunywea.
- Kaa kwenye benseni au bafu yenye maji vuguvugu kusafisha bawasiri na kupunguza maumivu.
Wakati mwingine bawasiri hujaa damu iliyoganda. Utahisi kitu kigumu kinachobonyea ndani na mshipa uliovimba. Uvimbe huu unaweza kutoa maumivu makali sana kiasi cha kutomruhusu mtu kukaa. Punguza maumivu kwa kuondoa damu hiyo iliyoganda:
Usikate na kuondoa bawasiri. Hii inaweza kusababisha kuvuja damu nyingi.
Jeraha wazi au michubuko kwenye unyeo
Muwasho, uchungu kama mwiba, au uvujaji damu kutoka kwenye unyeo unaweza kusababishwa na mchaniko mdogo wa ngozi. Hii kwa fikra ya haraka inaweza kudhaniwa kuwa bawasiri au minyoo. Mara nyingi mtu mzima mwenye muwasho kwenye unyeo huwa hana minyoo.
Michaniko hiyo kawaida husababishwa na kujifuta baada ya kujisaidia. Hali hiyo huzidishwa na kutosafisha unyeo vizuri baada ya kujisaidia.
- Usifute unyeo kwa kutumia mabunzi, gazeti, au vifaa vingine visivyo laini.
- Badala yake, tumia karatasi maalum ya kutawazia (toilet paper) au chombo cha maji kwa ajili ya kusafisha unyeo baada ya kujisaidia. Baada ya hapo, nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni.
- Oga mara kwa mara, na kusafisha unyeo wakati wa kuoga.
- Unaweza pia kujaribu krimu ya hydrocortisone, lakini usitumie kwa zaidi ya wiki au itaathiri ngozi
Maumivu kwenye njia ya haja kubwa
Wakati mwingine, watu hupatwa na uvimbe mwekundu na wenye maumivu pembeni na unyeo. Hujaa usaha na unakuwa aina ya jipu. Jipu linaweza kusababisha tundu kati ya unyeo na ngozi na unapaswa kukamuliwa mara moja. Toboa njia ya kutolea usaha karibu na unyeo, kadri iwezekanavyo. Angalia sura ya Ngozi, kucha, na matatizo ya nywele (inaandaliwa) kuhusu jinsi ya kukamua jibu.
AINA ZA BAWASIRI
A:BAWASIRI NDANI
Hii hutokea ndani katika mshipa wa haja kubwa wa ndani
Hutokea pale haja kubwa ikatishwapo na kurudi ndani wakati wa kujisaidia
B:BAWASIRI NJE
Hii hutokea eneo la nje la tundu la haja kubwa
na huambatana na maumivu makali au kuwasha sehem hii ya tundu la haja kubwa
Hivyo kupelekea mishipa ya damu kuvuja na kutengeza uvmbe katika tundu la haja kubwa au kuvuja damu katika eneo hilo la haja kubwa
CHANZO CHA UGONJWA HUU
-Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
-Kuharisha kwa mda mrefu
-Tatizo la kutopata choo laini au kujisaidia kinyesi kigumu
-Tatizo la umri mkubwa
-Uzito kupita kiasi
-Matumizi ya vyoo vya kukaa
DALILI ZA UGONJWA HUU
-Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
-Kujitokeza kwa uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
-Kujitokeza kwa kijinyama katika tundu la haja kubwa
Kujisaidia kinyesi chenye damu na kunuka kwa harufu mbaya sana
MADHARA YA UGONJWA HUU
-Kupata upungufu wa damu
-Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa
-Kutopata hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke -Kuathirika kisaikolojia
-Kukosa ari ya kufanya kazi na kutojiamini katika hadhara ya watu
JINSI YA KUEPUKA UGONJWA HUU
-Kutumia matunda na mboga za majani katika mlo
-Kunywa maji ya kutosha wakati na baada ya mlo
-Epuka kukaa chooni kwa mda mrefu
TIBA YAKE HOSPITALINI
Ugonjwa huu tiba yake ni kukukata uvimbe uliojitokeza katika tundu la haja kubwa
Lakini tiba hii si nzuri sana kwani hupelekea kujirudia tena kwa uvimbe pale mgonjwa akosapo kinga tosha
Pia hupelekea maumivu makali kwa mgonjwa
SULUHISHO LA UGONJWA HUU.
Suluhisho la ugonjwa huu umepatikana
Tiba lishe hizi zinatoa sumu zote zilizopo katika mwili kuondoa vimelea vya ugonjwa huu
Pia huzuia utokaji wa damu na pia kuondoa uvimbe na miwasho yote ijitokezayo katika tundu hili la haja kubwa
BAWASIRI NI UGONJWA HATARI KAMA HUTOUCHUKULIA HATUA YA TIBA MAPEMA
Post a Comment