Matatizo tisa yahusianayo na kulala na jinsi ya kukabiliana nayo
Hakuna atakaye kataa kuwa kulala ni kitu kinachopendwa na watu wengi. Hata kama ukikataa haitaondoa ukweli kuwa unatakiwa kulala baadae. Hata hivyo unajua kwamba kama hautalala zaidi ya masaa 72 una nafasi kubwa ya kufa. Na hili halina utani, imethibitishwa kisayansi.
Hivyo basi utafanya nini pale unakuwa na matatizo ya kiafya kisa kukosa usingizi wa kutosha? Kusaidia watu kutokana na tatizo hili la kukosa usingizi, nina kuletea hapa orodha ndogo athari za kulala vibaya na namna ya kuzikabili.
1. Kuamka ukiwa na maumivu kwenye mgongo
Maumivu ya mgongo ni moja ya athari ambazo wengi tunakumbana nazo. Hiyo ni jinsi ninavyoweza kuwaambia watu jinsi ya kutatua suala hili kwa njia ya haraka na rahisi. Ikiwa unaamka na maumivu ya mgongo, hakikisha unalala chali na kwa kutumia mto chini ya miguu yako ili kuunda Umviringo 'curvature' wa mwili wako. Ikiwa unachagua kulala kiupande upande basi weka mto katikati ya miguu yako.
2. Kujaribu kulala na Maumivu ya Shingo
Hapa pia kwenye tatizo hili unashauriwa kulala chali
3. Tatizo la Kukoroma
Jaribu kulala kiubavu ubavu au jaribu kulala na mto ambao utafanya shingo na kichwa kunyooka. Pia, kuna mazoezi maalum ambayo wanaweza kufanya ili kuimarisha misuli ya ulimi na koo.
4. Maumivu ya Mguu ya bila kutarajia (Leg Cramps)
Njia bora ya kuzuia maumivu ya miguu ambayo hukutarajia ni kujiwekea utaratibu wa kuinyoosha miguu kabla hujaenda kulala. Pia mazoezi ya yoga ya mara kwa mara yanaweza kusaidia
5. Matatizo ya Kiungulia/Maumivu ya miguu
Inua miguu yako kwa kuiweka juu ya mito, ambapo hili litawezesha damu kuelekea miguuni. Pia zuia utumiaji wa caffein masaa sita kabla ya kulala pia ifanyie miguu yako massage nzuri na kuisugua kwa chini. Amini au la, kulala ukiegemea upande wako wa kushoto huzuia chakula chako kisirudi, hivyo kuzuia kiungulia.
6. Maumivu ya bega
Kama unaamka na maumivu ya bega, inashauriwa sana kwako ulilale kwa tumbo (kifudifudi). Kwa mijubu wa CCN kulala chali ni njia nzuri kiafya ya kulala.
7. Tatizo la kushindwa kupata usingizi
Zima simu yako na kompyuta, usinywe kahawa yoyote masaa sita kabla ya kwenda kulala na jaribu kufanya mazoezi unapoamka na tena mchana. Hii itasaidia mfumo wako wa damu kuzunguka vizuri, na ni nzuri kwa afya. Au jaribu kusoma kitabu
8. Huwezi kulala kwa muda
Kwa kiasi kikubwa, zima simu yako kabla hujaenda kulala. Pia jaribu kupunguza kiasi cha pombe kabla ya kulala. Aidha, jotoridi la chumba chako lazima liwe karibu na nyuzi 68-70 Fahrenheit.
9. Tatizo la kushindwa kuamka asubuhi
Kila mtu ana tatizo hili, lakini ni rahisi sana kutatua. Muhimu ni marudio, jaribu kuanza kuamka kwa wakati mmoja kila asubuhi, hata mwishoni mwa wiki. Hata kulala mapema hakusaidii pia
10. Pumzika vizuri
Fuata maelekezo hayo hapo juu ili kuweza kulala vizuri usiku. Kama tatizo likiendelea muone daktari kwa maelekezo zaidi
Matatizo tisa yahusianayo na kulala na jinsi ya kukabiliana nayo
Reviewed by Cadotz media
on
October 22, 2020
Rating:
Post a Comment