je kuna tiba ya fibroids?

uvimbe kwenye kizazi(fibroids)Tatizo la uvimbe kwenye kizazi (fibroids) ni kubwa na linawatokea wanawake wengi sana. Inakadiriwa kwamba 75% ya wanawake hupata tatizo hili la fibroids katika kipindi flani cha maisha yao. Kwa mujibu wajarida la New England Journal of Medicine, kila mwaka zaidi ya wanawake 200,000 wanafanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi chote (hysterectomy) kutokana na tatizo hili la fibroids.

Fibroids ni nini?

Fibroids ni uvimbe usio wa sarataniambao hujitokeza kwenye kuta za mfuko wa mimba,uitwao uterusi, uvimbe huu husababisha kubadilika kwa shape na size ya kizazi na pia dalili zingine mbaya. Wanawake wengi huanza kupata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na uwepo wa uvimbe kwenye kizazi(fibroids . Ni jambo la msingi zaidi kwa wanawake wote kuchukua hatua katika kuzuia kutokea kwa fibroids.
Tafiti mbalimbali zinaonesha kwamba kuzuia au kutibu tatizo la kupanda kwa presha ya damu husaidia kupunguza hatari ya kupata uvimbe kwenye kizazi (fibroids). Utafiti uliofanyika katika chuo kikuu cha Havard unasema kuna uhusiano mkubwa kati ya presha ya damu na hatari ya kupata uvimbe kwenye kizazi(fibroids) kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi.

Unajuaje kama tayari una uvimbe kwenye kizazi (fibroids)

Je fibroids inaweza kusababisha kuvuja damu, maumivu ya mgongo na dalili zingine mbaya? Inawezekana kabisa lakini siyo kila mwanamke mwenye fibroids hupata dalili hizi, lakini pia uwepo wa dalili hizi siyo lazima kwamba una fibroids, unaweza kuwa na tatizo lingine la kiafya, ushauri mzuri ni kuonana na dactari haraka ili kupata vipimo. Zifuatazo ni dalili zinazojitokeza kwa wanawake wengi zaidi wenye uvimbe kwenye kizazi
  • Kupata Hedhi inayochukua siku nyingi kuanzia 7 na zaidi
  • Hedhi nzito
  • Kujiskia umeshiba mda mwingi
  • Maumivu ya nyonga
  • Kupata mkojo mara kwa mara na kushindwa kutoa mkojo wote kwenye kibofu.
  • Kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu
  • Kupata maumivu wakati watendo la ndoa
  • Maumivu chini ya mgongo na kwenye miguu.
  • Madhara mablimbali ya uzazi kamaugumba na mimba kutoka.

Uvimbe kwenye kizazi(fibroids) wakati wa ujauzito:  

Wakati mwingine mwanamke anaweza kupata fibroids akiwa kwenye ujauzito, ni dalili gani zinaweza kujionesha? Uvimbe kwenye kizazi(fibroids) inaweza kusababisha shida wakati wa kujifungua na kupelekea mwanamke kujifungua kwa upasuaji. Inaweza kupeleke ugumba pia kama tatizo ni kubwa sana kutokana na kwamba inakuwa vigumu kwa yai kurutubishwa na kisha kujishikiza kwenye ukuta wa uterus maana tayar kumesambaa uvimbe. Kwa wanawake ambao bado hawajazaa hushauriwa kutumia dawa ili kupunguza ukubwa wa uvimbe kabla ya kupata ujauzito, kama tatizo ni kubwa zaidi basi upasuaji hufanyika kabla ya kushika mimba. Kumbuka ni vizuri kufanya vipimo kabla hujaamua kushika ujauzito, hii itakusaidia kupunguza hatari ya kumpoteza mtoto.
Fibroids huweza kuongezeka ukubwa wakati wa ujauzito  kutokana na kiasi kikubwa cha homoni ya estrogen. Kuvuja damu na maumivu ya tumbo pia huweza kutokea kutokana na uvimbe kupoteza damu yake. Kwahiyo madactari wa wanawake hupendekeza mgonjwa kufanyiwa ultrasound mara kwa mara ili kufatilia maendeleo ya uvimbe.

Aina za uvimbe kwenye kizazi(fibroids)

Jina la kitabibu la fibroids ni leiomyoma au myoma. Ukubwa, mahali ulipo uvimbe na pia idadi ya vimbe hizi inachangia zaidi kwenye uwepo wa dalili mbaya aatakazopata mwanamke. Inawezekana kabisa kuwa na aina zaidi ya moja ya fibroid katika md mmoja kama zitatokea mahali tofauti tofauti kwenye uzazi wa mwanamke. Aina kuu za uvimbe kwenye kizazi(fibroids) ni kama zifuatazo
Intramural fibroids; ni aina marrufu zaidi na zinawatokea zaid wanakwake. Aina hii ya fibroid hukua na kumea kwenye misuli ya ukuta wa uterus. Kadiri zinavokua basi husababisha kupanuka au kuvutika kwa kizazi na kusababisha dalili kama hedhi ya muda mrefu inayoambatana na maumivu ya nyonga.
Subserosal fibroids: aina hii ya fibroids hukua nje ya ukuta wa mfuko wa mimba, wakati mwingine kuelekea kwenye kibofu cha mkojo. Aina hii ya fibroids huweza kusababisha maumivu ya chi ya mgongo kutokana na kwamba uvimbe huu unasukuma nerve za sipnal na kusababisha presha kubwa kwenye eneo la chini ya mgongo.
Submucosal fibroids: aina hii ya fibroid hukua karibu na ukuta wa uterus. inaweza kusababisha bleed ya muda mrefu na shida kwenye kushika ujauzito.
Cervical fibroids: hizi hukua kwenye tishu za mlango wa kizazi ambao huitwa cervix, hutokea mara chache sana ukilinganisha na aina zingine za fibroids.
Vihatarishi gani vinaongeza uwezekano wa kupata fibroids: dalili zifuatazo zinaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata uvimbe kwenye kizazi
  • Kurithi: kama mama au dada  yako aliwahi kuugua tatizo hili basi wewe pia utakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata uvimbe huu.
  • Umri: uvimbe kwenye kizazi (fibroids) hutokea zaidi kwa wanawake wanaokaribia kukoma hedhi kuanzia miaka 35 mpaka 40.
  • Lishe: matumizi ya vyakula vya wanga na sukari kupita kiasi huongeza hatari ya kupata fibroids
  • Uzito mkubwa na kitambi:wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wako kwenye hatari zaidi ya kupata fibroids .
  • Wanawake wenye shinikio kubwa la damu
  • Matumizi ya njia za kupanga uzazi:kama vidonge huongeza ukuaji wa fibroids kwani vidonge hivi huweza kupandisha homoni ya estrogen kwa wingi
  • Kubalehe mapema: wanawake wanaobalehe mapema na kuanza kupata hedhi chini ya miaka 10 wako kwenye hatari zaidi ya kuugua fibroids. Na pia
  • Wenye matatizo ya tezi ya Thairodi

Hatua saba za kuepuka na kutibu uvimbe kwenye kizazi (fibroids)

  1. Hatua ya kwanza: Epuka vyakula vyote vinavyoongeza ukubwa wa tatizo: vyakula vya kupiga chini ni kama vifuatavyo.
    • Vyakula vyenye mafuta mabaya na vilivyosindikwa: mfano nyama zilizosindikwa , baga na suausage huongeza mpambano(inflammation) na aleji. pia vyakula vilivyosindikwa vina kiasi kingi cha kemikali zinazowekwa ili kuongeza ladha hivo unapofanya uchaguzi wa nyama basi hakikisha unakula nyama kutoka kwa mnyama aliyefugwa kwa kula majani na siyo nafaka.
    • Maziwa yaliyosindikwa na kuhifadhiwa kwenye makopo:maziwa haya yana homoni nyingi za steroids na kemikali pia ambazo zinabadili ufanyaji kazi wa homoni zako za mwili na hivo kuongeza ukuaji wa fibroids.
    • Sukari: matumizi ya sukari kwa wingi iwe imesindikwa au ya asili huongeza mpambano kati ya tishu za mwili na kinga ya mwili na hivo kusababisha kuvimba au kututumka kwa tishu . hii huongeza maumivu na kupunguza uwezo wa kinga ya mwili. Unaweza kusoma vizuri uhusiano kati ya kuvurugika kwa homoni, kuongezeka uzito na uvimbe kwa kubonyeza hapa.
    • Wanga iliyokobolewa sana;katika kupambana na tatizo la uvimbe kwenye kizazi basi hakikisha unapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya vyakula vyenye wanga kwa wingi maana vyakula hivi hupandisha insulin nyingi kwenye damu na kuongeza hatari ya kupata uvimbe
    • Pombe na vinywaji vyenye caffeine. Matumizi makubwa ya pombe huongeza mcharuko au kututumka kwa tishu kwenye mwili . pombe pia huzorotesha kinga ya mwili na kusababisha uzito mkubwa na kuvurugika kwa homoni, unaweza kusoma makala yetu kuusu kuvurugika kwa homoni za kike na suluhisho lake jikoni kwa kubonyeza hapa.
  1. Hatua ya pili : Kula kwa wingi vyakula vya kukusaidia kutibu na kupunguza makali ya uvimbe.:vyakula hivi ni kama.
  • Vyakula vilivyoandaliwa pasipo matumizi ya kemikali (organic foods), sababu ni kama tulivoona hapo juu kwamba kemikali hizi zilizosheheni kwenye dawa za kuua wadudu zinaharibu mpangilio wa homoni na kusababisha seli za mwili kukua ovyo bila mpangilio. Kuhusu matunda na mbogamboga basi hakikisha unaosha kwa maji ya uvuguvugu yaliyochangnywa na vinegar hii husaidia kutoa kemikali za sumu zilizoganda kwa juu.
  • Mbogamboga za kijani : mboga za kijani zina viambata vinavyoondoa sumu kwenye mwili . pia mbogamboga za kijani zina Vitamin K kwa wingi sana ambazo husaidia katika kuganda kwa damu na hivo kusaidia kwenye bleeding.
  • Vyakula vyenye Beta carotene kwa wingi na madini ya chuma: mwili una uwezo wa kubadilisha beta carotene kuwa Vitamin A , na kazi ya vitamin A ni kujenga seli mpya zilizokufa na hivo kusaidia wenye fibroids. Baadhi ya vyakula vyenye beta carotene kwa wingi ni Nyanya, karoti na spinach. Kutokana na kwamba fibroid husababisha wanawake kupoteza damu nyingi kwa wakati fulani hivo ni muhimu kutumia vyakula kama maini, fogo, moyo ili kuongeza uzajishaji wa madini chuma ambayo husaidia katika utengenezwaji wa seli mpya nyekundu za damu.
  1. Hatua ya tatu: Jaribu kutumia baadhi ya virutubisho kwa ajili ya kupungeza ukubwa wa uvimbe;hakikisha unapata ushauri wa dactari kabla ya kuanza kutumia virutubisho hivi,
  • Mafuta ya samaki(fish oil) au mafuta ya flaxseed, kijiko kimoja kwa siku inaweza kusaidia kpunguza mcharuko kwenye mwili na hivo kusaidia kupunguza uvimbe kwenye kizazi
  • Vidonge vya vitamin B complex: hii husaidia kurekebisha kiwango cha homoni ya estrogen kwenye mwili na hivo kupunguza ukuaji wa uvimbe
4. Hatua ya nne. Kunywa chai tiba(herbal tea) unaweza utembelea kwenye stoo yetu ili kuweka oda: chai tiba zipo aina nyingi baadhi ya chai hizi ni pine pollen na kuding tea, chai hizi husaidia kubalansi homoni zako na hivo kusaidia katika kutibu uvimbe.
5.Hatua ya tano, Tumia mafuta ya castor: unapopakaaa mafuta ya castor kwenye tumbo lako husaidia kuongeza usafirrishaji wa damu na hivo kurahisisha utolewaji wa sumu haraka kwenye mwili. Watafiti wengi wa tiba wanaamni kwamba mrundikano wa sumu ndio unaopelekea kukua kwa fibroids. Jaribu pia detox package yetu ndani ya siku 30 ili kusafisha sumu kwenye mwili.
6. Hatua ya sita: Jiepushe na mzingira hatarishi yenye sumu : mazingira yenye sumu mbalimbali kama za kuua wadudu kwenye mazao, kemikali kwenye vyakula vya viwandani kuzuia ili visiharbike, kemikali za kuua magugu, na kemikali kwenye sabuni na mafuta , vyote hivi huchangia kukua kwa uvimbe kwenye kizazi (fibroids) kwa kuharibu mpangilio wa homoni. Na mwisho kabisa
7. Hatua ya saba: Fanya mazoezi ya kutosha walau mara 3 kwa week:  mazoezi husaidia kuzuia kutokea kwa uvimbe kwenye kizazi. Mazoezi hurekebisha presha ya damu, kuimarisha kinga, na kubalansi homoni zako 

Muhimu kwa Wagonjwa wa Fibroids

Kwa mwanamke mwenye uvimbe kwenye kizazi(fibroids), tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha kizazi na kurekebisha homoni zake. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 6 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama vimbe, maambukizi ya bacteria, PID na kuziba kwa mirija ya uzazi.
vidonge vya kusafisha kizazi
Vidonge hivi vinatumika kwa siku 24. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika siku 1,unaweka tena kidonge kingine. Gharama ni Tsh 100,000/=

Angalizo unapotumia Uterus Cleansing Pill’s

Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi, ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.