faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa





Miongoni mwa viungo maarufu sana na vinavyopendwa na watu wengi kutumika katika matumizi ya vyakula ni pili pili manga, kiungo hiki hutumiwa na watu wengi kwa kujua ama kutokujua kawa ina faida nyingi kiafya katika kuboresha afya ya mwil

FAIDA ZA KULA PILIPILI MANGA KIAFYA.

Pilipili manga mara nyingi hutumika kama kiungo kwa ajili ya kuongeza ladha kwenye chakula.
Lakini kiungo hicho kina faida kadhaa kiafya mwilini ambazo unapotumia unapaswa kuzijua faida zake.
Kabla ya kuangalia faida za pilipili manga mwilini tujue pilipili manga ina virutubisho gani.
Madini: Pilipili manga ina wingi wa madini ya Manganizi, Shaba, Magnesiamu, Kalsiamu, Fosforasi, Chuma na Potasiamu.
Vitamini: Pilipili manga ina wingi wa Vitamini B2, Vitamini B6, Vitamini C na Vitamini K.
Vilevile pilipili manga ina winga wa Nyuzi lishe, Protini na wanga.


FAIDA ZA PILIPILI MANGA.

Inaimarisha mfumo wa umeng’enyaji chakula:
Kwa kutumia pilipili manga inaongeza uzalishaji wa asidi tumboni ambayo inasaidia katika umeng’enyaji wa vyakula mbalimbali tumboni.
Pia pilipili manga inazuia uzalishaji wa gesi tumboni.

Kupunguza uzito.
Hasa magamba ya nje ya pilipili manga yanasaidia sana katika kuvunjavunja seli za mafuta mwilini.
Seli hizo huvunjwavunjwa na kutumika katika matumizi mengine ya mwili.
Hivyo pilipili manga ni njia salama ya asili ya kupunguza mafuta mwilini.

Tiba ya kifua na mafua.
Kwa mafua ya kawaida na kikohozi pilipili manga ni tiba nzuri ya asili.

Inapambana na magonjwa mbalimbali mwilini.
Pilipili manga ni msaada mwilini kwa kuwa inauwezo wa kuondoa bakteria wabaya. Pia pilipili manga inasaidia kuondoa lehemu mbaya na kusafisha mishipa ya damu (Ateri) .

Kuondoa sumu mbalimbali mwilini.
Pilipili manga ina viondoa sumu ambavyo husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwili ambazo zinaweza kuleta madhara mfano Saratani, pia kupunguza kasi ya mwili wako kuchoka na kuonekana mzee kabla ya umri na kupunguza kasi ya kupoteza kumbukumbu.
Inaboresha ufyonzaji wa virutubisho vingine mwilini.
Kuweka pilipili manga kwenye chakula si tu kuongeza ladha pia faida nyingine na kubwa ni kwamba pilipili manga inaufanya mwili kufyonza virutubisho kwenye chakula hicho kwa wingi zaidi tofauti na ungekula chakula hicho bila kutumia pilipili manga.

Tiba kwa vidonda vya tumbo:
Tafiti mbalimbali za kisayansi zimeonesha kuwa pilipili manga ina msaada katika kutibu vidonda katika mfumo wa chakula kutokana na viondoa sumu na viondoa uchochezi (Anti-inflammatory.) vilivyopo kwenye pilipili manga.

Tiba ya pumu (Asthma)
Kutokana na kuwepo kwa viondo uchochezi (anti-inflammatory) kwenye pilipili manga hivyo husaidia sana katika matatizo ya mfumo wa hewa kama vile Asthma.
Mengineyo:
Pia pilipili manga unaweza kuitumia kwa kutibu matatizo kama hernia(Ngiri), kukauka kwa sauti, kung’atwa na wadudu, maumivu ya jino au jino kuoza na matatizo ya macho.


ZINGATIA:
Pilipili manga inaweza kukusababishia chafya. Kwa mgonjwa ambaye amefanyiwa upasuaji wa tumbo epuka kuweka pilipili manga nyingi kwenye chakula.
Na kama utatumia pilipili manga ukaona dalili zozote za mzio (Allergy.) acha kutumia muone daktari.
AHSANTE.
LIKE page yetu kufahamu zaidi.


Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kujivunia huduma zetu pia tunakusogezea uchague unachokitaka katika menyu zetu. Cagua:- NEWS , HEALTH, MUSIC, LOVE, EVENTS, IT TRAIN
faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa faida ya pili pili manga mwilini katika kutibu magonjwa Reviewed by Cadotz media on September 02, 2020 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA