FAIDA YA KITUNGUU SAUMU -
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SWAUMU;
1.Kiua sumu
2.Kisafisha tumbo
3.Kiyeyusha mafuta(cholestro)
4.Huzuia mvilio wa damu
5.Kusafisha njia ya mkojo
6.Kutibu amoeba
7.Kuzuia kuhara damu(Dysentery)
8.Tumbo kushindwa kumeng'enya(Indigestion)
9.Gesi
10.Msokoto wa tumbo
11.Typhoid
12.Kidonda kilichooza
13.Dondakoo
14.Mabaka
15.Baridi yabisi(Rheumatisim)
16.Mishipa
17.Uziwi
18.Virusi vya homa ya mafua(Influenza)
19.Mafua
20.Saratani(Cancer)
21.Kifaduro
22.Kifua kikuu cha mapafu
23.Kipindupindu
24.Kutoa minyoo
25.Upele
26.Kuvunjavunja mawe katika figo
27.Mba kichwani
28.Kuupa nguvu ubongo
29.Kuupa nguvu fizi
30.Kuzuia meno kung'ooka
31.Nguvu za kiume
32.Maumivu ya kichwa
33.Kizunguzungu/kisunzi
34.Kutuliza maumivu ya meno
35.Kujenga misuli na kutia nguvu
36.Mkakamo wa ateri(Arteriosclerosis)
37.Shinikizo la damu
38.Kinga ya tauni na ukimwi
39.Magonjwa ya macho
Cadotz nijuze
Et Vitunguu kiboko kwa heshima ya ndoa?
Jibu: ndiyo
Kama jibu ni ndiyo, basi shaka hiyo haipaswi kuachwa bila kufanyiwa kazi. Ulaji wa vitunguu wenye kuzingatia maelekezo sahihi ya wataalamu wa lishe ni suluhisho tosha la namna bora ya ‘kunogesha’ ndoa, sababu ikiwa ni uwezo mkubwa wa chakula hicho katika kuupa mwili nguvu ya kushiriki jambo hilo kwa namna iliyo bora zaidi.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, ambazo baadhi zinachambuliwa kwa kina katika mitandao yenye habari za mapenzi na lishe kama wa ‘knowyourlove.wordpress’, ni kwamba ulaji wa vitunguu huwaongezea wawili uwezekano wa kufaidi ndoa yao kwa kuwapatia afya bora ya mwili kwa ajili ya mambo ya ndoa.
Inaelezwa kuwa vitunguu ni chanzo cha utitiri wa madini muhimu yanayohitaji mwilini, yakiwamo yale yanayosaidia kurekebisha kiwango cha sukari ambacho hutajwa kuwa chanzo cha kuyumbisha uwezo wa wawili katika kuridhishana pindi kisipodhibitiwa ;
kuimarisha afya ya moyo; kuzuia kansa; kuukinga mwili dhidi ya vidonda vya tumbo na pia kuzuia maambukizi ya vimelea mbalimbali vya magonjwa mwilini.
Kwa mujibu wa madaktari na pia wataalamu wa lishe, inaelezwa kuwa vitunguu ni chakula chenye kiasi kikubwa cha
‘aphrodisiac ‘, ambacho ni kiini lishe muhimu kwa masuala ya unyumba.
“Husaidia pia kuongeza nishati na kuimarisha viungo vya mwili vinavyohusika katika kuzalisha vichocheo vya tendo la ndoa.
Vitunguu pia huongeza mwilini kiwango cha testosterone na kusaidia kuongeza nguvu ya kushiriki tendo la ndoa,” mmoja wa madaktari aliiambia Nipashe kuhusiana na umuhimu wa vitunguu mwilini.
NAMNA YA KUVITUMIA
Inaelezwa kuwa faida za vitunguu mwilini ni nyingi, lakini zote hupatikana vyema pale mlaji anapozingatia maelekezo sahihi kabla ya kuvijumuisha katika mlo wake.
Miongoni mwa njia zinazoweza kumpa faida mlaji mwenye nia ya kupata ufumbuzi wa tatizo la nguvu za kiume (kwa kina baba), kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ni pamoja na kuvitafuna vikiwa vibichi au mcghanganyiko wake baada ya kupondwa.
“Unaweza kukata kitunguu katika vipande vinne na kuvisaga kwa blenda (blender). Baada ya hapo, kunywa juisi yake ambayo husaidia sana kumuongezea mlaji uwezo wa kushiriki tendo la ndoa,” alisema mtaalamu mwingine kabla ya kuongeza kwa kutoa tahadhari:
“Juisi (ya kitunguu) ni chungu na hivyo unapaswa kunywa polepole ili kutoushitua mfumo wa mwili kwa kuinywa ghafla na kwa haraka.
Kuongeza vitunguu swaumu katika juisi ya vitunguu vya kawaida pia ni jambo zuri na husaidia sana kuongeza nguvu za tendo la ndoa.
Mchanganyiko wake unaweza kuitwa dozi ya mapenzi kutokana na faida zake nyingi mwilini kwa ajili ya kufanikisha tendo la ndoa.”
Aidha, inaelezwa kuwa njia nyingine nzuri ya kutumia vitunguu ni kwa kuvikata vipande vidogo vidogo na kuvikaanga kwa jibini, kisha kuvila pamoja na asali kama chakula cha kwanza kuingia mwilini asubuhi.
Mchanganyiko huu unatajwa vilevile kuwa nafaida kubwa za afya ya tendo la ndoa na pia huupa mwili kiasi kikubwa cha kiinilishe cha ‘aphrodisiac’.
Vitunguu husaidia pia kuongeza urembo katika ngozi za walaji wake, hasa kina mama.
FAIDA YA KITUNGUU SAUMU -
Reviewed by Cadotz media
on
February 04, 2019
Rating:
Post a Comment