Faida za mmea wa aloe vera au mshubiri


1. Huondoa uvimbe katika jicho

Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe.

2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito

Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote.

3. Hutibu bawasiri

Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili, ndiyo hiyo hiyo pia husaidia kutibu au kupunguza maumivu ya bawasiri. Chana tawi la aloe vera freshi na upate jeli yake, kisha pakaa eneo linalosumbuliwa na bawasiri mara mbili mpaka tatu kwa siku kwa wiki kadhaa hasa kama bawasiri imejitokeza sehemu ya nje hadi hapo uvimbe huo utakapopotea.

4. Ni tiba kwa matatizo ya tumbo

Kama utainywa,hutibu vidonda vya tumbo na kiungulia, na kwa ujumla ni kuwa husafisha mfumo wote wa mmeng'enyo wa chakula. Chukua jeli ya aloe vera nusu kikombe (ml 125) changanya na maji ya kawaida nusu kimbe tena kupata ujazo wa robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 1 kujitibu matatizo ya tumbo kama kuuma, kuondoa sumu, kuunguruma, kuhara na hata kutibu malaria.
Madhara ambayo yameripotiwa kutokana na kunywa aloe vera ikiwa freshi ndani ya tumbo ni pamoja na kuharisha na matatizo kwenye figo.

5. Huziimarisha kucha dhaifu

Kwa taratibu pakaa majimaji ya aloe vera juu ya kucha zako sehemu zote juu na chini kila siku na uzitazame baada ya siku kadhaa uone zitakavyokuwa zimerudisha ule uzuri na ugumu wake wa mwanzo.

6. Huondoa Makeup

Kwa usalama kabisa huondoa makeup kwenye jicho na ni nzuri kwa ngozi laini inayozunguka jicho lako.

7. Husafisha ngozi na kuondoa alama
zitokanazo na kuungua na jua
Chunusi,ukurutu na kuungua kwa ngozi kutokana na jua vyote hivi vinatibika kirahisi kwa kutumia aloe-vera. Pakaa mara 2 hadi 3 kwa siku katika ngozi mpaka uone umepona kabisa. Mu-aloe vera pia una sifa ya kupoza kama ilivyo
menthol ambayo unaufanya Mu-aloe vera kuwa dawa ya asili nzuri zaidi katika kutibu alama zitokanazo na kuungua na jua.

8. Ni jeli ya asili ya kunyolea na baada ya kunyoa

Aloe Vera ni dawa ya asili katika kutibu michubuko asante kwa vimeng'enya vyake ambavyo huwa na kiasi kingi cha maji ambayo ni mhimu kuzuia kukauka kwa ngozi. Wakati unanyoa ndevu pakaa jeli ya aloe vera na hata baada ya kunyoa pakaa kama after shave jel kuzuia na kuponya michubuko itokanayo na kunyoa.

9. Huondoa makunyanzi na mikunjo ya ngozi

Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo zote zinapatikana katika aloe vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na kuiacha katika hali ya umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe-vera na mafuta ya asili ya nazi utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na unyevunyevu katika ngozi.
Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya maji ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki na unyevunyevu muda wote.

10. Hutibu homa na mafua

Jeli ya Aloe Vera huongeza kinga ya mwili. Mu-aloe-vera una viinilishe vingi sana mhimu kwa afya ya binadamu. Ina Vitamini A, B, C, na E. Mmea huu una orodha ndefu ya madini mhimu kwa mwili na vimeng'enya vingine mhimu.

11. Vitamini B12 kwa wale wasiotumia nyama (Vegans)

Matumizi makuu ya aloe vera kimatibabu ni kusaidia na kuboresha uundwaji wa bakteria wazuri. Kwa kuongezea aloe vera huwa na jumla ya madini ambayo bakteria huyahitaji katika kutengeneza Vitamini B12.

12. Huongeza nguvu mwilini

Matumizi mengine ya kitabibu ya mmea wa mu aloe vera au mshubiri kwa kiswahili chake hasa, ni kuongeza usawa wa nguvu mwilini. Hii ni kutokana na uwepo wa vitamin b 14 na viinilishe vingine

Endelea kutembelea cadotz blog inayokuunganisha na madaktari bingwa
Faida za mmea wa aloe vera au mshubiri Faida za mmea wa aloe vera au mshubiri Reviewed by Cadotz media on September 25, 2018 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA