Zifahamu hapa faida ya kutumia chenza kila mara kiafya
Chenza ni moja ya tunda lenye ladha nzuri sana na lenye kupendwa na watu wengi wakiwemo watoto na watu wazima pia
Tunda hili wengi wetu tumekuwa tukilitumia sana huenda kutokana na kupenda ladha yake tu, lakini hili ni moja ya tunda ambalo pia lina faida nyingi katika miili yetu.
Ila siku ya leo nitakueleza japo kwa uchache faida zitokanazo na chenza kama ifutavyo;
1. Tunda hili ni tamu lina faida nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwemo kuongeza vitamin C,
2. Pia linazuia kuvuja damu katika fizi kwa watu wenye matatizo ya kutokwa na damu katika fizi za meno yao.
3. Vilevile tunda hili lina imarisha mifupa, linaongeza nguvu katika miusuri nakuondoa maumivu ya viungo.
4. Pia linaondoa baridi yabisi, linaondoa viuvimbe chini ya tumbo, linasaidia kuondoa mawe katika figo na kibofu, linatibu unene na mirija ya damu na kutibu udhaifu wa macho.
Mara nyingi watalamu wa afya wanashauri kula tunda lenyewe lililowiva tu kwa sababu hili ndilo limesheeni wingi wa faida lukuki kama ambavyo tumeeleza hapo juu.
Zifahamu hapa faida ya kutumia chenza kila mara kiafya
Reviewed by Cadotz media
on
June 08, 2020
Rating:
Post a Comment