Maambukizi Katika Mfumo Wa Mkojo (U.T.I)
Viungo hivyo hujumuisha figo, mirija inayopitisha mkojo kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu (ureta), kibofu na mrija wa kutolea mkojo nje ya mwili (urethra).
Maambukizi haya yamekua yakiwasumbua watu wengi wa jinsia zote. Wanawake ndio wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na tatizo hili kutokana na maumbile yao. Watoto pia wanaweza kuathiriwa na tatizo hili hasa wale wa kike chini ya umri wa miaka miwili na mara nyingi dalili zake kwa watoto huwa si wazi.
Asilimia kubwa tatizo hili husababishwa na vimelea vya Escherichia coli (E. Coli), vimelea hawa kwa kawaida huishi katika utumbo wa binadamu bila kusababisha mdhara yoyote ila wapohamishwa kwenda sehemu nyingine huleta madhara (normal frola).
Vimelea hawa hufika kwenye mirija ya kutolea mkojo pale ambapo muhusika anashindwa kujisafisha vizuri baada yakujisaidia haja kubwa kwani hutolewa nje ya mwili pamoja na haja kubwa, vilevile kwa njia ya kujamiaana. Pia kuna aina nyingine za vimelea ambazo husababisha tatizo hili ukiacha na E.Coli. vimelea hawa husambaa kelekea kwenye kibofu na wakati mwingine hufika kwenye figo ikiwa mgonjwa hatatibiwa mapema.
Wanawake wanaathiriwa zaidi na tatizo hili kwa sababu wana mrija mfupi wa kutolea mkojo pia ukaribu uliopo kati ya sehemu ya kutolea haja kubwa na mrija wa kutolea mkojo. Pia wanawake wanaojamiiana maranyingi wako katika hatari ya kupata tatizo hilo.
Sababu nyingine ni kama kupungukiwa kinga mwilini, wagonjwa wliowekewa mirija ya kukojelea kwa muda mrefu(catheter),vile vile kuziba kwa njia ya mkojo.
Aina za U.T.I
zimegawanyanyika kutokana na kiungo kinachokuwa kimeathirika. Kwenye figo ambapo kwa jina la kitaalam inaitwa pylonephritis, kwenye kibofu inafahamika kama cystitis na kwenye urethra inafahamika kama urethritis.
Dalili za UTI ni pamoja na:
-kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine kupata mkojo kidogo,
-maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo ambayo yanakua kama yanaunguza( burning sensation),
-maumivu ya kichwa pamoja na homa,
-kukojoa mkojo wenye harufu kali pia unaweza kuwa umechanganyikana na damu au unakua na ukungu Fulani,
-maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
-Wakati mwingine mwili kukosa nguvu pia kukosa hamu ya kula.
Ni vizuri kufanya vipimo kabla ya kuanza kutumia dawa mara nyingi kipimo kinachotumika ni kuupima mkojo wa mgonjwa (urine analysis)
Maambukizi ya mfumo wa mkojo yanatibika kutumia dawa aina antibayotiki ambazo mgonjwa ana takiwa anywe dozi iliyokamilika na kwa usahihi. Tiba hii hutegemeana na umri, ujauzito na kuwepo kwa hali zingine. Pia huzingatia na usambaji wa vimelea yaani UTI kali na isiyo kali.
UTI isipotibiwa inaweza kusababisha madhara makubwa kama kuharibika kwa figo, kwa wajawazito wanaweza kujifungua watoto wenye uzito pungufu vile vile mirija ya mkojo kupungua sababu ya makovu.
Jinsi ya kujikinginga na maambukizi katika njia ya mkojo, mwanamke inatakiwa ajifunze jinsi ya kujisafisha baada ya kujisaidia haja kubwa; badala ya kujisafifisha kutoka nyuma kwenda mbele inatakiwa aanze mbele na amalizie nyuma ili kuepusha kinyesi kufika katika njia ya mkojo.
Pia kunywa maji mengi husaidia mtu kupata haja ndogo mara kwa mara hivyo kupunguza idadi ya vimelea katika njia ya mkojo na hivyo kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi katika njia ya mkojo.
Kutokukaa na mkojo kwa muda mrefu, hakikisha kila unaposikia haja ndogo hakikisha unaenda kujisaidia. Pia kubadili nguo za ndani mara kwa mara kwa wanawake husaidia na sisiwe zinabana sana. Bila kusahau kusafisha vyoo kabla na baada ya kujisaidia.
Matunda yanayoweza kusaidia UTI:
-Juice ya Malimao
-Juice ya machungwa
-Mananasi
-Epo
-Vitunguu saumu
-Tangawizi
Maambukizi Katika Mfumo Wa Mkojo (U.T.I)
Reviewed by Cadotz media
on
June 14, 2019
Rating:
Post a Comment