DAWA YA MWAROBAINI, FAIDA KIAFYA


Mwarobaini (Azadirachta indica ) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko India na
Burma. Mwarobaini hushamiri zaidi katika
nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame.
Jina “mwarobaini” linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini. Majani na mibegu ya mwarobaini imekuwa ikitumiwa kama tiba kwa miaka maelfu huko nchini India na hivi sasa inatumiwa katika sehemu mbalimbali duniani likiwemo bara la Afrika .
Wanasayansi wa nchi za Magharibi hutumia pia mti huu kwenye tiba na utafiti. Mwanzoni mwa mwaka 2005, serikali ya India ilipeleka kesi mahakamani kupinga hatua ya mamlaka ya leseni ya Ulaya (European Patent
Office) kutoa leseni kwa Wizara ya Kilimo yaMarekani na kampuni ya kimataifa ya
WR Grace kumiliki haki ya kutengeneza na kuuza dawa ya ukungu inayotokana na mwarobaini.
Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k. Matawi yake hutumiwa kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.
Mafuta ya mibegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni. Kiziduo cha mibegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu wanaoharibu mimea shambani.




TIBA YA MUARUBAINI


1.TIBA hii hutunza meno na kuondoa harufu mbaya mdomoni. Kwa watu wanaopenda kula vitu vyenye sukari kama maziwa na mikate ambavyo vikiganda mdomoni husababisha sukari na kuathiri. Wapenzi na wapenda soda ambazo zina kiasi kikubwa cha sukari, wanatakiwa kutumia mwarobaini.
Miswaki: Tumia tawi dogo kutoka kwenye mti huu ambalo lina kemikali ya asili na kusafisha au kutunza fizi za meno.
Magamba ya mwarobaini hutumiwa kutengeneza baadhi ya dawa za meno zinazouzwa madukani.


2. Hutunza ngozi

Mwarobaini ni mzuri katika kutibu magonjwa mengi ya ngozi yanayoambukiza na yasiyoambukiza.
Unaweza pia kuutumia katika kutibu madhara yatokanayo na chakula au dawa.
Oga: Kwa asili, Wahindi wengi huoga maji ya moto yaliyolowekwa majani ya mwarobaini ili kuweka kinga kwenye ngozi zao.
Mafuta: Chukua gramu 100 za mafuta ya ngozi ya kawaida uongeze gramu 10 za mafuta ya mwarobaini, paka utaona mafanikio.


3.Vidonda vya kuungua
vilivyochunika:

Chukua majani ya mwarobaini kiganja kimoja kisha changanya na maji lita moja, chemsha kwa dakika 20. Baada ya hapo chuja yakiwa bado ya moto kisha yapooze, osha sehemu iliyoungua. Maji haya yanasaidia kuzuia maambukizi.


Labda tuangazie macho japo kwa uchache kwa kuona maajabu ya mti huu kama ifuatavyo.

1. Mwarobaini ni dawa ya kuua minyoo yote tumboni,

2. Hutubu homa, hasa zile homa za usiku

3. Mwarobaini hutibu kikohozi.

4. Mwili kuwaka moto.

5.kuharisha pamoja na tatizo la vidonda vya tumbo. Chukua majani ya mmea huu kisha yatafune bila kujali uchungu yaliyo nayo.


6.Mwarobaini hutubu matatizo ya macho.
Ili kutibu matatizo ya macho Unachotakiwa kufanya ni kufuata maelekezo kama amabayo nitaeleza hapo chini.


7.magonjwa mbalimbali ya ngozi hutibika pia kwa kutumia mti huu wa mwarobaini.
Kwa kutibu magonjwa hayo na magonjwa mengineyo unachotakiwa kufanya:

Chemsha majani 40 ya mti wa 
mwarobaini kwa muda wa dakika kumi tano, baadae acha mchanganyiko huo upoe, kisha chuja kwa ajili ya matumizi. Unaweza ukanywa mchanganyiko huu asubuhi na jioni. Kwa kiwango cha kikombe kimoja cha chai. Kikombe kimoja asubuhi na kingine jioni.

DAWA YA MWAROBAINI, FAIDA KIAFYA DAWA YA MWAROBAINI, FAIDA KIAFYA Reviewed by Cadotz media on February 02, 2019 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA