Siri ya ujana katika fenesi na faida zake kiafya

Siri ya ujana katika fenesi

JE, unataka ngozi yako iendelee kuwa nyororo pasi na mikwaruzo?. Na je, unataka ngozi ya mwili wako iwe bado inaita kwa kuwa nyoofu pasi na mikunjo hata kama tayari umeshakula chumvi nyingi?. Kama jibu ndiyo, jawabu lake ni pamoja na kuanza kuwa mlaji mzuri wa tunda la fenesi.
Sababu Tido kukwepa jela
Wavamia eneo la Makaburi na kujenga nyumba za makazi
Tido aachiwa huru kesi ya kusababishia hasara serikali
Dkt. Fatma Mrisho aipongeza MSD

HABARI KUBWA
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Nipashe uliohusisha mahojiano na baadhi ya wataalamu wa masuala ya lishe na pia kupitia tafiti mbalimbali za kiafya, imebainika kuwa fenesi ni njia mojawapo nzuri ya kuwafanya walaji wadumu kwa muda mrefu katika muonekano wao wa ujana.
Katika uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo huo wa kipekee wa tunda la fenesi unatokana na wingi wa virutubisho vyenye kuipa afya ngozi ya mlaji.

“Watu wengi hawajui kuhusu siri ya tunda la fenesi… ni kwamba, lina virutubisho vingi kwa ajili ya kuipa ubora ngozi ya mlaji, kuwapa muonekano wa urembo wa asili kina dada na pia kuulinda mwili dhidi ya magonjwa mengi,” mmoja wa madaktari katika Hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa aliiambia Nipashe jana.
Aidha, imeelezwa zaidi kuwa tunda hilo ambalo kitaalamu huitwa ‘Artocarpus heterophyllus’, huwasaidia kina mama walioko kwenye ukomo wa hedhi kwa kuipa afya misuli ya damu na hivyo kuwaweka katika hali nzuri zaidi.

Akizungumza na Cadotz  jijini Dar es Salaam jana, Mtaalam wa Lishe,

Dk. Emmanuel Mgonja, alisema fenesi ni tunda muhimu kwa afya kwa sababu limejaaliwa kuwa na virutubisho ambavyo ni pamoja na vitamini A, C, B - complex, vitamin B6, folic acid, niacin na riboflavin.

Pia alisema siri ya tunda hilo nia pamoja na kuwa na wingi wa madini muhimu kwa mwili wa binadamu ambayo ni pamoja na potassium, magenesium, manganese na chuma.

Kadhalika, Dk. Mgonja alisema fenesi lina protini, mafuta, wanga na ‘antioxidants’ ambazo ni muhimu kwa kuondosha vijisumu mwilini. Pia ni chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na mafuta yenye lehemu.

Kutokana na utajiri wake huo wa virutubisho, ndipo fenesi huwa na faida nyingi kwa walaji ikiwa ni pamoja na kuzifanya ngozi zao muda wote ziwe angavu, nyororo na muonekano wa ujana hata kwa kina mama waliokoma hedhi.
“Fenesi linapoliwa vizuri na wanawake wenye umri mkubwa huifanya misuli yao kufanya kazi vizuri kwa kiwango kinachostahili na linasaidia kurutubisha ngozi zao,” alisema.
Pia alisema ulaji wa tunda hilo husaidia kusisimua misuli ya damu ambayo ilikuwa imelegea na kuifanya ifanye kazi vizuri.
Alisema kwa virutubisho vilivyomo, tunda hilo huzuia magonjwa nyemelezi na kuukinga dhidi ya maumivu ya mifupa yanayosababishwa na ukosefu wa madini ya chuma.
ULAJI MZURI WA FENESIDk. Mgonja alisema ni vizuri nusu saa kabla ya kupata mlo, kula walau gramu 200 za fenesi kwa siku.
“Unashauriwa kula gramu 100 asubuhi na gramu 100 jioni … na zote ziliwe nusu saa kabla ya kula chakula au unaweza kutengeneza juisi na kuinywa nusu saa kabla hujala chakula. Juisi hiyo uinywe mara mbili au tatu kwa siku,”alisema Dk. Mgonja.


ZIFUATAZO NI FAIDA ZA FENESI.
Ngozi ya FENESI

yaani ile ganda lenye vipelevipele. Ukichemsha na kunywa utapata faida zifuatazo kiafya.

1)hushusha sukari mwilini kwa haraka sana.

2)hutibu pumu

3)huimalisha mifupa

4)huongeza kinga ya mwili na kukufanya usisumbuliwe na magonjwa

5)ni kinga ya cancer yaani hutaumwa na cancer

6)huimalisha mmeng'enyo wa chakula kwa waathirika wa HIV

NA ILE NGOZI TAMU YA NJANO AMBAYO WATU HULA

1)huzuia upungufu wa damu kwa mlaji wa FENESI

2)huleta vitamin A na B6

3)huleta nguvu


MBEGU ZAKE

Kausha mbegu zake juani na utwange upate unga kisha uhifadhi kwa matumizi yenye faida zaidi.

1)ukichanganya na maziwa ukapaka sehemu ngozi imeharibika asubuhi na jioni kwa wiki mbili sehemu hiyo itakuwa safi.

2)hufanya USO kuwa soft. Changanya unga wa mbegu za fenesi katika maziwa flesh na asali update paste nzito. Kisha paka usoni asubuhi na jioni basi uso utakuwa softi sana.

3)huongeza nguvu za kiume
Changanya unga wa mbegu ktk maziwa flesh asubuhi na jioni tendo la ndoa halitakusumbua na shemeji atakupa shikamo.

4)chemsha mbegu zake kisha unywe supu yake na utafune mbegu hizo. Huondoa presha kwa mwenye presha ya kupanda
Pia ukitafuna mbegu huleta protini
Siri ya ujana katika fenesi na faida zake kiafya Siri ya ujana katika fenesi na faida zake kiafya Reviewed by Cadotz media on January 30, 2019 Rating: 5

No comments

Ndugu ahsante kwa kuitembelea Cadotz, Endelea kufurahia huduma zetu pia Tunakusogezea Cadotz uchague unachokitaka katika menyu zetu.
Bofya chini

MIZIKI | MAPENZI | AFYA